Tutuko zosta yana historia ndefu iliyorekodiwa, ingawa rekodi za zimeshindwa kutofautisha kati ya malengelenge yanayosababishwa na VZV na yale yanayosababishwa na ndui, [16] hali ya erogoti na erisipela. Ilikuwa ni mwishoni mwa karne ya kumi na nane ndipo William Heberden alibaini njia ya kutofautisha kati ya tutuko zosta na ndui, [64] na tutuko zosta haikuweza kutofautishwa na erisipela hadi mwisho wa karne ya kumi na tisa. Katika mwaka wa 1831, Richard Bright alitoa nadharia tete kuwa ugonjwa huo ulitoka kwenye ganglioni ya shina la uti wa mgongo, na jambo hili lilithibitishwa katika makala ya 1861 yaliyoandikwa na Felix von Bärunsprung. [65]